Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki zote za binadamu kwenye ibara 30 za tamko la haki za binadamu haziachanishiki

Kamati ikitayarisha muswada wa kimataifa kuhusu haki
UN Photo.
Kamati ikitayarisha muswada wa kimataifa kuhusu haki

Haki zote za binadamu kwenye ibara 30 za tamko la haki za binadamu haziachanishiki

Haki za binadamu

Ibara ya 30 ya tamko la kimataifa la  haki za binadamu linasema vipi? Jebra Kambole wakili kutoka Tanzania anakuelezea kwa muhtasari.

Leo tarehe 10 Desemba mwaka 2018 ni kilele cha maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani ambapo katika mfululizo wa wetu wa kuchambua ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu, tunatamatisha kwa kuangazia ibara ya 30. Ibara hii inaeleza baya kuwa haki zote zilizomo kwenye tamko hilo lililopitishwa tarehe 10 Desemba mwaka 1948 huko Paris, Ufaransa haziachanishiki. Je hii ina maana gani, wakili Jebra Kambole, kutoka Tanzania ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu anafafanua.