Utekelezaji wa ibara 13 Kenya ni mzuri licha ya changamoto

19 Novemba 2018

Ibara ya 13 ya tamko la haki za binadamula Umoja wa Mataifa ambalo linatimiza miaka sabini mwaka huu inasema, kila mtu ana haki ya uhuru wa kutembea na kuishi ndani ya mipaka ya nchi yake - Na kila mtu ana haki ya kuondoka na kurudi nchini mwake.

Haki hii inalindwa na serikali kwa mujibu wa katiba za nchi wanachama walioridhia tamko hilo.

Moja ya nchi hizo ni Kenya ambapo kwa mujbu wa Robi Chacha, Afisa kampeni usalama na haki za bindamu katika shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International, nchini Kenya,  haki hii ipo kwenye katiba ya Kenya na kwa maoni yake utekelezaji wake unazingatiwa.

Hata hivyo Bwana Chacha ametoa mifano ya wakati ambapo mtu anayimwa haki hii ikiwa anahatarisha usalama katika nchi yake au anaugua ugonjwa ambao ni wa kuambukiza. Bwana Chacha ameeleza hayo akizungumza na Grace Kaneiya ambapo anaanza kwa kufafanua ibara ya 13.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter