Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania imepiga hatua katika kutekeleza baadhi ya haki za washitakiwa: Henga

Nakala ya awali ya haki za binadamu (Picha ya UM/Greg Kinch)

Tanzania imepiga hatua katika kutekeleza baadhi ya haki za washitakiwa: Henga

Haki za binadamu

Tanzania imepiga hatua katika utekelezaji wa baadhi ya haki za binadamu ikiwemo kuhakikisha haki za  washitakiwa kudhaminiwa, au tutokuchukuliwa kuwa na hatia hadi itakapothibitishwa. 

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania, Anna Henga alipozungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Bi Henga amesema pamoja na changamoto ambazo bado zinajitokeza kwa watu kutofahamu haki zao kisheria, au wapi pa kufikisha malalamiko  na nini cha kufanya, hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya kuridhia tamko la haki za binadamu na kuingiza vipengee kwenye katiba zimesaidia utekelezaji wa tamko hilo  la Umoja wa Mataifa lililopitishwa yapata miaka 70 iliyopita ikiwemo ibara ya 11 inayosema  “kila mtu aliyehukumiwa ana haki ya kudhaminiwa na kutohesabiwa hatia mpaka ithibitishwe”. Akifafanua hatua zilizochukuliwa na serikali kusaidia  hili.