Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanafamilia hapaswi kushinikizwa kujiunga au kutojiunga na kikundi - UDHR

Mipango ya uwezeshaji wanawake ni hatua muhimu zitakazoleta manufaa kwa jamii
UNDP Angola/ M. Casal
Mipango ya uwezeshaji wanawake ni hatua muhimu zitakazoleta manufaa kwa jamii

Mwanafamilia hapaswi kushinikizwa kujiunga au kutojiunga na kikundi - UDHR

Haki za binadamu

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, #UDHR likitimiza miaka 70 mwezi disemba mwaka huu wa 2018, harakati mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kukumbusha binadamu haki zao za msingi zilizotajwa bayana ndani ya nyaraka hiyo yenye ibara 30.

Nchi zilizotia saini na kuridhia tamko hilo, zinakuwa ni sawa na kufunga pingu ya kwamba zitatekeleza haki hizo na la msingi ni kwamba haki hizi zinachukuliwa kwa umoja wake badala ya kuchagua moja na kuacha nyingine.

Miongoni mwa haki hizo ni ile ya kujiunga au kutojiungana kikundi chochote ambayo imeelezwa bayana katika ibara ya 20 ya tamko hilo. Katika mfululizo wetu wa  uchambuzi wa ibara hizo leo mtaalamu wetu ni wakili Aloyce Komba kutoka Tanzania ambaye katika mahojiano na Arnold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anachambua ibara hiyo kwa kuanza na ainisho.