Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya baadhi ya wafanyakazi ughaibuni inasikitisha- Emma Mbura

Hali ya baadhi ya wafanyakazi ughaibuni inasikitisha- Emma Mbura

Pakua

Ibara ya 23 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasema kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi anayoifanya, kufanya kazi katika mazingira salama na ulinzi dhidi ya ukosefu wa ajira. Kipengele cha pili kwenye ibara hiyo kinasema kuwa kila mtu, bila kubaguliwa ana haki ya kulipwa mshahara sawa kwa kazi sawa. Ibara hiyo inakwenda mbali zaidi na kusema kuwa kila mtu ana haki ya ujira unaofaa kwa ajili ya matumizi yake na familia kuwawezesha kuishi kwa utu na nyongeza kwa ajili ya ulinzi wa kijamii. Kipengee cha nne na cha mwisho kinasema kuwa kila mtu ana haki ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi kwa ajili ya kulindwa kwa maslahi binafsi. Licha ya kwamba haki hii ipo katika sheria ya baadhi ya nchi ambazo zimeridhia, lakini wakati mwingine utekelezaji wake unakuwa na doa. Je ni kwa vipi? Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango/ Grace Kaneiya/Emma Mbura
Audio Duration
5'14"
Photo Credit
UN Picha/Greg Kinch