Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ibara ya 18 ni haki ya kimataifa-Shaheed

Viongozi wa dini mbalimbali.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Ibara ya 18 ni haki ya kimataifa-Shaheed

Haki za binadamu

Kila mtu ana haki ya kufuata dini, imani au fikra zozote za kidini kwani hii ni haki ya kila mtu kote ulimwenguni.

Hiyo ni kwa mujibu wa Ahmed Shaheed, mtaalam maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya dini au imani akifafanua ibara ya 18 ya tamko la haki za binadamu.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Bwana Shaheed amesema haki hiyo inalenga wanaoamini Mungu, wasioamini walio na imani zisizo za kidini kwani

(Sauti ya Shaheed)

“Kwa upande mmoja wa haki hii ambao unalenga imani, hiyo haiwezi kuingiliwa na mtu au mamlaka ya taifa. Upande mwingine wa haki hiyo ni yale yanayojitokeza katika kufurahia haki hiyo katika faragha au kwa kujumuika hadharani na watu wengine katika ibada, kusherehekea na kufuata dini. Kuna uwezekano wa kunyimwa haki hii katika misingi ya usalama wa umma, amani, afya na maadili na iwapo inaingilia haki za wengine lakini ni lazima misingi hiyo izingatia sheria za kimataifa."