Skip to main content

Tume ya Wataalamu imeonya vikwazo dhidi ya JKK (DRC) bado vinaendelea kuharamishwa.

Tume ya Wataalamu imeonya vikwazo dhidi ya JKK (DRC) bado vinaendelea kuharamishwa.

Tume ya Wataalamu wanaohusika na vikwazo dhidi ya JKK (Congo-DRC) wamedhihirisha ripoti mpya yenye kuthibitisha kuharamishwa vikwazo vya silaha vinavyoendelezwa na wageni pamoja na raia katika Congo-DRC.

Ripoti ilionya ya kuwa biashara haramu, na ya magendo, ya silaha, risasi na baruti inayofanyika ndani ya nchi ni kitendo kinachohatarisha kabisa juhudi za kimataifa za kurudisha amani. Ripoti ilisema hali hii vile vile inapaliliwa na tabia karaha ya kufadhilia fedha yale makundi yanayoharamisha vikwazo, makundi ambayo yamekutikana kuiba mali ya asili ya Kongo-DRC, kama vile almasi na yale maadini hatari yajulikanayo kama uranium na radium.

Wataalamu wa UM wamependekeza kuanzishwe ushirikiano wa karibu na wa haraka kati ya jamii ya kimataifa na Shirika la Ulinzi wa Amani la MONUC ili kuhakikisha tatizo hili linakabiliwa vilivyo, hasa ilivyokuwa JKK hivi sasa imo katika harakati za kuandaa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwisho wa mwezi.