Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imefanikiwa kurudisha makwao katika Sudan ya kusini wahamiaji 262.

UNHCR imefanikiwa kurudisha makwao katika Sudan ya kusini wahamiaji 262.

Shirika la UM Linalohudumia Wahamiaji (UNHCR) wiki hii limesaidia kwenye huduma za kuwarudisha Sudan ya kusini wahamiaji 262 kutoka Uganda ya Kaskazini. Idadi hii inajumlisha wahamiaji 10,000 kati ya 350,000 waliopo mataifa jirani na Sudan wanaotegemea kurudishwa makwao na UNHCR.