Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inahimiza kufadhiliwa msaada wa dharura kuokoa maisha ya raia katika Pembe ya Afrika.

UNICEF inahimiza kufadhiliwa msaada wa dharura kuokoa maisha ya raia katika Pembe ya Afrika.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF)limeripoti kuwa linahitajia kufadhiliwa haraka msaada wa dola milioni 43 kukidhia mahitaji ya dharura ya kiutu kwa mamilioni ya wanawake na watoto wadogo waliokabiliwa na tatizo haribifu la ukame katika eneo la Pembe ya Afrika.