Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Usomali aanza ziara ya mataifa saba kushauriana suluhu ya amani

Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Usomali aanza ziara ya mataifa saba kushauriana suluhu ya amani

Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Usomali, Francois Lonseny Fall wiki hii ameanza ziara ya nchi saba, zikijumuisha Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Misri, Sudan pamoja na Uganda na Yemen kwa makusuddio ya kushauriana na viongozi wa mataifa hayo juu ya taratibu za kurudisha usalama na amani katika Usomali.