Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa CITES juu ya udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu

Mkataba wa CITES juu ya udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu

Ofisi Kuu ya taasisi ya Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mimea Pori na Wanyama Wanaohatarishwa Kuangamizwa - mkataba ambao hujulikana kwa umaarufu kama Mkataba wa CITES - hivi karibuni ilichapisha taarifa muhimu yenye kubainisha mapendekezo karibu 40 yanayotakikana yatekelezwe na nchi wanachama ili kurekibisha kanuni za kuendesha biashara ya viumbe pori katika soko la kimataifa.

Kutokana na uharibifu wa kasi wa viumbe vya baharini, pamoja na uharibifu wa rasilmali za misitu unaofanyika ulimwenguni jumuiya ya kimataifa imelazimika kuyazingatia kidharura masuala haya sugu ambayo bado yanaendelea kutaharakisha walimwengu. Miongoni mwa matatizo haya yanayolitatanisha bara la Afrika ni zile kadhia za uharibifu mbadhirifu wa biashara haramu ya pembe za ndovu.

David Morgan ni Mkuu anayehusika na Kitengo cha Kumudu Huduma za Kisayansi za Mkataba wa CITES, na alifanya mahojiano na Idhaa ya UM ambapo aliyahimiza mataifa ya Afrika kushirikiana ili kuimarisha kanuni za kuboresha hifadhi ya biashara ya pembe za ndovu kwenye ukanda wao, na pia katika ulinzi wa tembo waliopo kwenye maeneo yao.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.