Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

Vikosi Mseto vya UM/UA vya Kulinda Amani Darfur (UNAMID) vimearifu askari 45 wa Kombania ya Usafiri Wastani ya Jeshi la Ethiopia waliwasili karibuni katika Darfur Magharibi. Kombania hii ya majeshi ya Ethiopia itatumiwa kugawa shehena za mizigo na vifaa baina ya kambi za walinzi wa amani wa UNAMID, ikijumlisha ugawaji wa maji na matangi ya nishati, na vile vile kuwapatia wanajeshi usafiri.

Kuachiwa kwa Raisi wa Mauritania kwapongezwa na KM

Ijumatatu KM alitoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake, iliyopongeza ripoti za kuwachiwa kutoka kifungo cha nyumbani Raisi wa Mauritania, Sidi Ould Cheikh Abdallahi, ambaye serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu.

Mkutano wa Sirte ni wa daraja ya juu, asema mjumbe wa SADC

Kwenye mkutano mkuu wa siku tatu, wa kiwango cha mawaziri, uliofanyika kwenye mji wa Sirte, Libya wiki iliopita, kujadilia miradi ya kutunza maji kwa kilimo na kuzalishia nishati katika Afrika, kulikubaliwa rai ya kuchangisha mabilioni ya dola kukidhia mipangop hiyo ya maendeleo.

Hapa na Pale

Baraza la Usalama Ijumatatu limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za MONUC, yaani lile Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK, kwa mwaka mmoja zaidi.Vile vile Baraza lilipiga kura ya kuendeleza vikwazo dhidi ya JKK mpaka mwisho wa Novemba 2009.~