Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Ukraine

Watoto wakimbizi kutoka Somalia wakiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya ambako WFP inawapatia misaada ya dharura.
WFP/Rose Ogola

Majanga yanavyozidi kushamiri isiwe kisingizio cha kusigina haki za mtoto- UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hususan zile za mtoto wametoa taarifa ya pamoja hii leo huko Geneva, Uswisi wakisema  majanga ya kiafya, kibinadamu na yale  yanayohusiana na tabianchi yakizidi kuongeza changamoto kubwa duniani kila uchao kama vile ukimbizi wa ndani, ukatili wa kingono na njaa, serikali lazima zikumbuke kuwa watoto wana haki kamilifu za kimsingi za kibinadamu na kwamba haki hizo zinapaswa kulindwa.

Leo ni Siku ya uhuru wa Ukraine hapa ni mjini Kyiv
© UNDP Ukraine/Krepkih Andrey

Miezi sita ya vita nchini Ukraine haya ni baadhi ya yaliyofanywa na WFP

Hii leo imetimia miezi sita rasmi tangu kuanza kwa vita baina ya Ukraine na Urusi baada ya Urusi kuivamilia Ukraine vita ambayo si tu imeleta madhara na maafa kwa Ukraine bali dunia kwa ujumla ikiwemo kupandisha bei za mafuta na chakula. Katika siku hiii tuangalia machache yaliyofanywa na moja tu la mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa lile la Mpango wa Chakula duniani WFP katika kuwasaidia wananchi wa Ukraine.

Sauti
3'5"