Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UN wa nishati ya atomiki waelekea kwenye kituo cha nyuklia Ukraine

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi anaongoza timu ya ujumbe wa wataalamu wa IAEA katika ziara yao rasmi nchini Ukraine kwenye Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Zaporizhzhya.
IAEA/Dean Calma

Amani na Usalama

Kikosi cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya nishati ya atomiki leo kimeelekea kwenye kituo cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzya nchini Ukraine, baada ya miezi kadhaa ya mvutano ulioongezeka kati ya vikosi vya Ukraine na Urusi, ambavyo vimeshtumu kila mmoja kwa kukishambulia kwa makombora kinu hicho. 

Kikosi cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya nishati ya atomiki kilielekea Jumatatu kwenye kituo cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzya nchini Ukraine, baada ya miezi kadhaa ya mvutano ulioongezeka kati ya vikosi vya Ukraine na Urusi, ambavyo vimekuwa vikishutumiana kila mmoja kwa kukishambulia kwa makombora kinu hicho. 

Katika ujumbe wa Twitter, Rafael Grossi, mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA amesema kwamba anajivunia kuongoza ujumbe wa msaada na usaidizi wa shirika hulo kwenda Zaporizhzya, kwenye mtambo ambao umekuwa ukidhibitoiwa na vikosi vya Urusi tangu muda mfupi baada ya uvamizi wao nchini Ukraine. 

"Siku imefika ya kulinda ulinzi na usalama wa mtambo huo, ambao ni mkubwa zaidi barani Ulaya” ameandika bwana Grossi maoni yake yakiambatana na picha yake na wafanyakazi wengine 13 wa IAEA, kabla ya kuanza safari yao. 

Mara tu timu ya IAEA inapowasili Zaporizhzya baadaye wiki hii Bwana. Grossi ameonyesha kwamba vipaumbele vya wataalam ni pamoja na kufanya tathmini ya uharibifu na kutathmini kama mifumo ya ulinzi na usalama inaendelea kufanya kazi. 

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi anaongoza timu ya ujumbe wa wataalamu wa IAEA katika ziara yao rasmi nchini Ukraine kwenye Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Zaporizhzhya.
IAEA/Dean Calma
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi anaongoza timu ya ujumbe wa wataalamu wa IAEA katika ziara yao rasmi nchini Ukraine kwenye Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Zaporizhzhya.

Usalama wa kinu hicho na wafanyakazi ni kipaumbele 

Kazi zingine za dharura pia ni pamoja na kuangalia hali ya wafanyikazi wa Ukraine ambao bado wanaendesha mtambo huo, ambao unahifadhi vinu sita kati ya 15 vya nyuklia nchini humo. 

Katika wiki na miezi ya hivi karibuni, Bwana Grossi ametoa wito mara kwa mara wa fursa ya kufikia kicho cha Zaporizhzya, huku pia akiwahimiza wanajeshi wote kurudi nyuma kutoka kwenye kinu hicho, ili kisiwe mlengwa. 

Wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama uliochochewa na mzozo huo mapema mwezi huu, mkurugenzi mkuu wa IAEA alisema "wakati ni jambo la msingi hasa kutokana na kutokuwa na uhakika wa hali na tishio kubwa linalowezekana la ajali ya nyuklia.” 

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Rafael Mariano Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, anaelekeza kwenye Kiwanda cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine kwenye ramani.
© IAEA/Dean Calma
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Rafael Mariano Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, anaelekeza kwenye Kiwanda cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine kwenye ramani.

Ukaguzi wa ana kwa ana unahitajika 

Taarifa zilizopokelewa kutoka Ukraine na Urusi kuhusu hadhi ya kituo hicho zimekuwa zinazokinzana limesema shirika la IAEA likibainisha wakati huo, kuhusu uendeshaji wake na uharibifu unaoendelea. 

Ziara rasmi ya pekee ya amana kwa ana Zaporizhzya ingeweza kufanya uwezekano wa kuthibitisha tathmini hizi, amesema Bwana Grossi akiongeza kuwa wataalam wa IAEA pia walihitaji "kuthibitisha hali ya vinu na orodha ya nyenzo za nyuklia ili kuhakikisha kutochepushwa kutoka kwa matumizi ya amani”. 

Usafirishaji nje kupia bahari nyeusi unaendelea 

Katika hatua nyingine inayohusiana, mpango unaoongozwa na Umoja wa Mataifa wa kupata mauzo ya nje ya nafaka za Ukraine na vyakula vingine kutoka bandari za nchi hiyo umeripoti kuwa karibu tani milioni 1.25 sasa zimesafirishwa. 

Taarifa ya Jumapili kutoka kwa kituo cha uratibu wa pamoja (JCC) inayohusisha Ukraine, Urusi, Türkiye na Umoja wa Mataifa kiliripoti kuwa jumla ya safari 114 zimewezeshwa hadi sasa (62 za ndani na 52 za nje), tangu makubaliano hayo yatiwe saini tarehe 27 Julai mwaka huu mjini Istanbul Uturuki. 

Mfanyakazi akitoa chakula cha msaada katika ghala la WFP huko Sana'a
WFP/Mohammed Awadh
Mfanyakazi akitoa chakula cha msaada katika ghala la WFP huko Sana'a

Yemen itanufaika pia 

Meli tatu za kibiashara ziliidhinishwa kusafiri siku ya Jumatatu zikiwa na zaidi ya tani 70,000 za vyakula. 

Meli hizo zilijumisha Karteria, ikitoka Yuhzny huko Pivdennyi na kuelekea Uturuki ikiwa na tani 37,500 za ngano. 

"Nafaka hii inanunuliwa na shirika la mpango wa chakula duniani (WFP), kimebainisha kituo cha uratibu cha  JCC.  

Kimeongeza kuwa ngano hiyo "Itasagwa kuwa unga huko Uturuki na kisha itapakiwa kwenye meli mpya itakayoelekea Yemen. Meli ya pili, Amani M, ilipaswa kusafiri kutoka Odesa hadi Constanta, Rumania, ikiwa na tani 24,485 za mahindi, ya tatu, Ash Baltic, ilipangwa kuondoka kutoka Odesa kwenda El Dekhela, Misri, ikiwa na tani 11,000 za mahindi.”