Wataalamu wa UN wa nishati ya atomiki waelekea kwenye kituo cha nyuklia Ukraine
Kikosi cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya nishati ya atomiki leo kimeelekea kwenye kituo cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzya nchini Ukraine, baada ya miezi kadhaa ya mvutano ulioongezeka kati ya vikosi vya Ukraine na Urusi, ambavyo vimeshtumu kila mmoja kwa kukishambulia kwa makombora kinu hicho.