Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Urusi yatumia kura turufu kuzuia azimio la kupinga utwaaji wake wa maeneo ya Ukraine

Taswira ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipokutana kujadili amani na usalama hususan Ukraine
UN /Rick Bajornas
Taswira ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipokutana kujadili amani na usalama hususan Ukraine

Urusi yatumia kura turufu kuzuia azimio la kupinga utwaaji wake wa maeneo ya Ukraine

Amani na Usalama

Azimio lililowasilishwa na Marekani kwa ushirikiano na Albania kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo ili kupinga kitendo cha Urusi kujitwalia maeneo ya Ukraine limegonga mwamba baada ya Urusi kupinga kwa kutumia kura yake turufu.

Wanachama 10 kati ya 15 wa Baraza hilo waliunga mkono huku Gabon, China na Brazil wakijiengua kwenye upigaji kura.

Kuya ya hapana ilikuwa ni ya Urusi na ambayo imetumia kura turufu au Veto na hivyo azimio haliwezi kusonga kokote.

Huu ni wakati wa kusimama kidete na Chata ya UN

Akiwasilisha azimio hilo, Mwakilishi wa kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Linda Thomas-Greenfield, amesema huu si wakati wa kukaa kando, bali huu ni wakati wa kutetea Chata ya Umoja wa Mataifa kwa misingi na malengo yake.

Amesema iwapo Urusi inachagua kujilinda yenyewe dhidi ya uwajibikaji, “basi tutapeleka hatua mbele kwenye Baraza Kuu ili kutuma Moscow, Urusi ujumbe usiotetereka ya kwamba dunia iko kwenye upande wa kutetea uhuru na eneo la mipaka.”

Balozi Thomas-Greenfield pia amegusia kwamba, mapema leo dunia imeshuhudia Rais Vladmir Putin wa Urusi akisherehekea ukiukwaji huu dhahiri wa sheria ya kimataifa kwa kuandaa hafla kujipongeza yeye nyuma ya kura ya maoni isiyo halali.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Marekani amesema Rais huyo wa Urusi anajitukuza na kukumba himaya ya Kisovieti na kwamba huo ulikuwa ni mwanzo.

“Sote tulivyoketi kwenye ukumbi huu, na kuzingatia kwa machungu azimio hili, Rais Putin kwa maringo anakandamizi kwa mbele ya nyuso zetu maadili tunayoshirikishana.

Balozi Thomas-Greenfield amesema ni wakati wa kusimama kidete na kutetea imani yetu ya pamoja.

Nani alitarajia Urusi ipitishe rasimu kama hii ?

Akihutubia wajumbe, Balozi Vasily Nebenzya, ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa amesema kwamba nchi yake inalazimika kusema kuwa baadhi “ya wenzetu kwenye Baraza hili wamefikia kiwango chao kipya cha chini kabisa na hata masalia kidogo ya utu kwenye ukumbi hii yamekiukwa.”

Amesema hafahamu mfano wowote ambapo Baraza la Usalama lingaliweza kupitisha azimio ambalo moja kwa moja linalaa mmoja wa wajumbe wake.

“Hebu niambieni, mnadhara kwa umakini kabisa Urusi inaweza kuzingatia na kuunga mkono rasimu ya aina hiyo,” alihoji.

Akizungumza kwa niaba ya Ukraine, Sergiy Kyslytsya, amesema “mwakilishi wa Urusi amefuata hatua za mkuu wake wa Moscro, ambako maonesho ya vikaragosi yaliandaliwa leo ili kujaribu kupinga jambo la wazi: kwamba utawala vamizi na wenye kusaka mambo mapya nchini Urusi unaelekea kushindwa.

Kyslytsya pia amesema kuwa “sitatolea ufafanuzi uongo ambao hauna nafasi kwenye ukweli.”

Hapo jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alizungumza na wanahabari jijini New York, Marekani akiitaka Urusi isitekeleza mpango wake wa kutwaa maeneo ya Ukraine.