Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi yoyote inayojielewa ingefanya kama tulichofanya kulinda watu wetu :Urusi

Waziri wa Mambo ya Nje Sergey V. Lavrov wa Urusi anahutubia mjadala mkuu wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu.
UN Photo/Cia Pak
Waziri wa Mambo ya Nje Sergey V. Lavrov wa Urusi anahutubia mjadala mkuu wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu.

Nchi yoyote inayojielewa ingefanya kama tulichofanya kulinda watu wetu :Urusi

Masuala ya UM

Tulikuwa tunakabiliwa na nchi za magharibi zilishindwa kuafikiana na huku serikali ya Ukriane ikiwa katika vita dhidi ya wananchi wake huko mashariki, Urusi haikuwa na "chaguo" isipokuwa kuanzisha kile ambacho Serikali inataja kama operesheni yake maalum ya kijeshi, Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo.

Waziri huyo wa mambo ya nje amesema operesheni iliyozinduliwa tarehe 24 Februari mwaka huu 2022 ilikuwa imefanywa ili kuwalinda Warusi wanaoishi katika mikoa ya Donetsk na Luhansk ya huko Ukraine, na kuondoa vitisho kwa usalama wa Urusi.

Ameeleza muungano wa kijeshi wa NATO unaoongozwa na Muungano wa Ulaya na Marekani umeundwa mara kwa mara katika eneo hilo tangu kile alichoelezea kama "mapinduzi ya umwagaji damu" ya "serikali ya sasa ya Kyiv", mwaka 2014.

"Nina hakika kwamba Serikali yoyote iliyo huru, inayojiheshimu ingefanya vivyo hivyo kama sisi, serikali ambayo inaelewa wajibu wake kwa watu wake."

Lavrov alishutumu nchi za Magharibi kwa "kupiga kura ya maoni" mwishoni mwa wiki hii katika kura ya maoni inayoendeshwa huko Donbas na maeneo mengine yanayodhibitiwa na Urusi juu ya kuwa sehemu Urusi, akipinga kwamba watu huko walikuwa wakifuata tu agizo kutoka Kyiv, lililowataka "kutoka nje na kwenda Urusi”.

Marekani inafanya kila nchi kama uwani kwake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi alisema migogoro inayozunguka vita inazidi kuongezeka, na hali ya kimataifa inazidi kuzorota kwa kasi, lakini badala ya kuwa na mazungumzo ya kuaminiana na kutafuta maelewano, nchi za Magharibi "zinadhoofisha imani katika taasisi za kimataifa" na kuhamasisha mwelekeo mbaya ndani ya Umoja wa Mataifa pia.

Alisema Marekani inajaribu kugeuza ulimwengu wote kuwa "kama uwani kwake", na pamoja na washirika wake, kuwaadhibu wapinzani kutokana na mtazamo wake wa dunia, kupitia kile alichokiita "vikwazo haramu vya upande mmoja" ambavyo vinakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kuwaumiza raia masikini. katika nchi maskini zaidi, zikilenga dawa zao, chanjo na uagizaji wa chakula kutoka nje.

'Uchochezi'

Majaribio ya Marekani kulazimisha migawanyiko, kuwaambia mataifa "ama uko pamoja nasi au kinyume nasi", ilimaanisha kuwa badala ya "kuwa na mazungumzo ya ukweli" badala yake kulikuwa na "taarifa potofu, maonesho machafu na uchochezi".

Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Urusi alimsifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa kuhamasisha juhudi za kuondokana na mzozo wa chakula na nishati duniani unaochochewa na vita. 

Lakini pia amelaumu mataifa ya Magharibi kwa usimamizi mbovu wa kiuchumi katika janga hilo, akidai kuwa vikwazo dhidi ya nchi yake ni sawa na "vita vya kiuchumi dhidi ya Urusi."

Alipongeza Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi wa kukomboa chakula na mbolea kutoka Ukraine, na Urusi, ili kupunguza mfumuko wa bei na usambazaji, lakini alisema nchi masikini bado hazifaidiki, na alikosoa tena Marekani na Jumuiya ya Ulaya kwa kutoondoa "vikwazo" kikamilifu. kwa mauzo ya nje ya Urusi alisema yalinaswa katika bandari za Ulaya.

Madai ya "Russophobia"

Lavrov aliliambia Baraza Kuu kuwa sasa kulikuwa na "vita vya msalaba vya nchi za Magharibi dhidi ya wale wanaopinga", huku NATO ikiiona Urusi kama tishio kwa utawala wake wa eneo hilo na kwingineko.

Zaidi ya hayo, chuki  dhidi ya Urusi ama Russophobia, imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, na mataifa ya Magharibi hayakuficha azma yao ya kuishinda kijeshi Urusi, na kujaribu "kuharibu na kuivunja Urusi… chombo, ambacho kimekuwa huru sana.”

Okoa ubinadamu kutoka kuzimu

Alizionya nchi zaidi ya Ulaya na Amerika Kaskazini, kwamba muungano wa Magharibi, katika juhudi za kulazimisha utashi wake, ulikuwa unatafuta kupanua ushawishi na nguvu zaidi katika Bara la Asia, Amerika ya Kusini na Afrika, na akamalizia matamshi yake kwa kunukuu ushawishi mkubwa na busara za Katibu Mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa, Dag Hammarskjöld "Umoja wa Mataifa haukuumbwa ili kuwapeleka wanadamu peponi, bali kuokoa wanadamu kutoka kuzimu."

"Haya ni maneno ya maana sana. Yakituomba, kuelewa wajibu wetu binafsi na wa pamoja wa kuweka mazingira kwa ajili ya maendeleo ya amani na maelewano kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo, na kila mtu anatakiwa kuonyesha nia ya kisiasa kwa hilo.” Alisema Lavrov

Akimalizia hotuba yake kwa njia ya upatanishi, na kuashiria mustakabali mzuri wa umoja wa pande nyingi, alisema ana hakika kwamba utulivu wa ulimwengu unaweza kuhakikishwa, kwa kurejea "chimbuko la diplomasia ya Umoja wa Mataifa", kwa kuzingatia kanuni muhimu. ya "usawa huru wa Nchi".