Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna dalili za kusitishwa kwa mapigano Ukraine: Guterres

Taswira ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  ambako wajumbe wamekutana leo kujadili amani na usalama Ukriane.
UN /Loey Felipe
Taswira ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambako wajumbe wamekutana leo kujadili amani na usalama Ukriane.

Hakuna dalili za kusitishwa kwa mapigano Ukraine: Guterres

Amani na Usalama

Akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambao hii leo wamekutana kujadili kuhusu vita nchini Ukraine, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alielezea masikitiko yake makubwa kwamba hakuna dalili za kusitishwa kwa mapigano.

Mkutano huo wa ngazi ya juu unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna kwa kuwa nchi yake ndio inashika urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Septemba.

Katika miezi ya hivi karibuni, Bwana Guterres amebainisha "tumeshuhudia mateso na uharibifu usioelezeka. "Kama nilivyosema tangu mwanzo, vita hivi visivyo na maana vinaleta madhara makubwa  kwa Ukraine na kwa ulimwengu wote. Wazo la mzozo wa nyuklia, ambalo haliwezi kufikiria, limekuwa mada ya mjadala."

Guterres amesema mataifa yote, ambayo yana silaha za nyuklia, yanapaswa kuthibitisha kujitolea kwao kwa kutotumia na kuondoa kabisa silaha hizo.

Ameeleza pia kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya ripoti za mipango ya kuandaa kile kinachoitwa "kura za maoni" katika maeneo ya Ukraine ambayo hayako chini ya udhibiti wa serikali kwa sasa: unyakuzi wowote wa eneo la jimbo na serikali nyingine kwa nguvu au kwa sababu ya tishio la serikali yake ni ukiukaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana kando mwa UNGA77 kujadili amani na usalama duniani hususan Ukraine
UN /Loey Felipe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana kando mwa UNGA77 kujadili amani na usalama duniani hususan Ukraine

Mateso ni kwa wengi duniani

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitoa muhtasari wa matokeo ya kusikitisha ya mapigano hayo hadi sasa na kueleza kuwa maelfu ya raia wa Ukraine, wakiwemo mamia ya watoto, wameuawa na kujeruhiwa, takriban watu milioni 14 wamelazimika kukimbia, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

“Hali itazidi kuwa mbaya zaidi wakati majira ya baridi yanapokaribia, António Guterres ametabiri, hasa huku usambazaji wa gesi na umeme ukipungua.”

Uharibifu wa dhamana ya vita hivi unahisiwa katika nchi kadhaa zinazoendelea ambazo tayari zinajitahidi kupona kutokana na janga la coronavirus">COVID-19 na zinakabiliwa na majanga ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

UN inafanya nini

Vifurushi vya chakula vya WFP vinagawiwa kwa watu walioathiriwa na vita katika Mkoa wa Kharkiv kwa ushirikiano na Shirika la Msalaba Mwekundu la Ukraine.
© WFP/Ukrainian Red Cross/Yurii Chornobuk
Vifurushi vya chakula vya WFP vinagawiwa kwa watu walioathiriwa na vita katika Mkoa wa Kharkiv kwa ushirikiano na Shirika la Msalaba Mwekundu la Ukraine.

Umoja wa Mataifa unafanya kila jitihada kutafuta njia ya kutoka katika hali hii.

Katibu Mkuu huyo ameeleza ambavyo amekuwa akisafiri mara kwa mara katika eneo hilo, alitembelea Ukraine naUrusi, na huko alizungumza na Rais Zelensky na Rais Putin. Pamoja na washirika wa misaada ya kibinadamu.

Umoja wa Mataifa umetoa msaada kwa karibu watu milioni 13 wenye uhitaji, ndani ya nchi ya Ukraine yenyewe na kwa wakimbizi ambao walijikuta katika nchi nyingine.

Kipengele muhimu, Guterres anaamini, ni mkusanyiko wa ukweli na usitishwaji wa hali zote za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uhasama. Hivyo, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu inafuatilia na kurekodi matokeo ya vita hivi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, orodha ya uhalifu inatisha “mauaji ya watu wengi, unyanyasaji wa kijinsia, mateso na "matendo ya kinyama na ya kudhalilisha raia na wafungwa wa vita." Ripoti za hivi karibuni za mazishi ya pamoja huko Izyum zimesababisha, kulingana na mkuu wa Umoja wa Mataifa, hofu kubwa.

Guterres amesema wahusika lazima wawajibishwe kwakufunguliwa kesi kwenye mahakama za haki na ambazo ni huru. "Waathirika na familia zao wana haki ya kupata haki zao, kufidiwa na kuwepo na masuluhisho na marekebisho. Na Umoja wa Mataifa una mifumo muhimu ya taratibu hizo za kisheria,” António Guterres alisisitiza.

Nchi wanachama wa Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa zikiwemo Ghana, Falme za Kiarabu, Gabon, Albania, Uingereza nazo zilikuwa miongoni mwa waliozungumza kulaani uvamizi wa urusi na kueleza hakuna nchi ipo juu ya sheria na mikataba ya Umoja wa Mataifa inapaswa kuheshimiwa.