Miezi sita ya vita nchini Ukraine haya ni baadhi ya yaliyofanywa na WFP

Leo ni Siku ya uhuru wa Ukraine hapa ni mjini Kyiv
© UNDP Ukraine/Krepkih Andrey
Leo ni Siku ya uhuru wa Ukraine hapa ni mjini Kyiv

Miezi sita ya vita nchini Ukraine haya ni baadhi ya yaliyofanywa na WFP

Msaada wa Kibinadamu

Hii leo imetimia miezi sita rasmi tangu kuanza kwa vita baina ya Ukraine na Urusi baada ya Urusi kuivamilia Ukraine vita ambayo si tu imeleta madhara na maafa kwa Ukraine bali dunia kwa ujumla ikiwemo kupandisha bei za mafuta na chakula. Katika siku hiii tuangalia machache yaliyofanywa na moja tu la mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa lile la Mpango wa Chakula duniani WFP katika kuwasaidia wananchi wa Ukraine.

Tarehe 24 Mwezi February mwaka huu 2022 wananchi wa Ukraine waliamka na kushuhudia makombora yakipiga majengo mbalimbali hali iliyozua taharuki na mamilioni ya watu hususan wanawake, wazee na watoto kukimbilia nchi jirani au mikoa jirani kusaka hifadhi ili kuokoa maisha yao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP siku chache baada ya kuzuka vita lilianza kusambaza chakula, kwanza lilianza na mikate kwa wala waliokuwa wamekwama nchini Ukraine na kisha baadae kuendelea na utuoaji wa vifurushi vilivyo sheheni aina mbalimbali za vyakula vya kuwapatia wananchi lishe ikiwemo vyakula vya protini, wanga, mafuta, na mpaka sasa zaidi ya tani 64,000 za vyakula vimesambazwa nchini humo. WFP pia inafahamika kwa kuongoza kutoa usaidizi wa fedha taslimu katika maeneo yenye mizozo. Mpaka sasa zaidi ya dola milioni 200 zimetolewa kwa familia zaidi ya Ukraine. Na kwa nchi jirani ya Moldova ambapo mamia ya waukraine walikimbilia huko familia 11,000 zilizo wahifadhi wakimbizi wa Ukriane zimepata mgao wa fedha taslimu kwa ajili ya kuwawezesha kununua chakula na mahitaji mengine muhimu. Na kwa wakimbizi wa ndani vocha za chakula za dola 13 kwa mtu mmoja kwenye kila familia zimenufaisha takriban watu 64,000. Taifa la Ukriane ni wakulima na kabla ya vita kuzuka walikuwa wakizalisha chakula cha kutosha kulisha watu milioni 400 kwa mwaka. Kuzuka kwa vita kulifunga usafirishaji nje ya nchi bidhaa kutoka nchini Ukraine na Urusi mataifa yanayotegemewa na soko la dunia katika uzalishaki wa Ngano na mahindi na hivyo kupandisha bei marafuku ya mazao hayo kutokana na uhaba wa mazao. Baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hatimaye Ukraine imeanza kusafirisha nafaka na wiki iliyopita Meli ya WFP iliyosheheni tangi 23,000 za nafaka imeondoka Ukraine kupeleka chakuna katika pembe ya Afrika ambako kumekumbwa na ukame mkali. Kuimarisha uzalishaji wa chakula nchini Ukriane si tu utawanufaisha wananachi wa Ukraine bali pia kuleta manufaa kwenye soko la Kimataifa ndio maana WFP inaendelea kufanya kazi na mamlaka za mitaa, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta ya kibinafsi kurejesha upatikanaji wa chakula, kuleta utulivu wa huduma za taasisi na kuendeleza shughuli za kiuchumi ili kupunguza hatari kwa muda mrefu.