UN yalaani mauaji ya raia 200 yaliyofanywa na ISIL Syria
Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la kutisha lililofanywa na magaidi wa ISIL kwenye maeneo yanayokaliwa na raia wengi huko jimbo la As-Sweida kusini-magharibi mwa Syria.
Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la kutisha lililofanywa na magaidi wa ISIL kwenye maeneo yanayokaliwa na raia wengi huko jimbo la As-Sweida kusini-magharibi mwa Syria.
Zaidi ya watoto 7,000 wamepoteza maisha yao au wamejeruhiwa na kuachwa na ulemavu wa kudumu kutokana na mgogoro unaoendelea nchini Syria.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea mjini Sweida Syria siku ya Jumatano.
Wakimbizi wa Syria takriban 171 wanaoishi nchini Jordan wamekuwa wanasumbuliwa na matatizo ya figo na tiba yake ni gharama kubwa wasiyoweza kuimudu hadi sasa ambapo habari njema imewaletea matumaini mapya.
Mjumbe maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Angelina Jolie, amerejea tena nchini Iraq na kushuhudia jinsi wakimbizi kutoka Syria wanavyohaha kuishi ikiwemo kulea watoto wao wenye mahitaji maalum.
Shirika la afya duniani, WHO limetoa wito kwa ulinzi wa vituo vya huduma za afya huko kusini mwa Syria sambamba na kutoa fursa zaidi kwa watoa misaada kuingia eneo hilo.
“Muziki uliokoa maisha yangu” kauli hiyo yenye matumaini na yenye lengo la kuwahamasisha wakimbizi wanaopitia zahma mbalimbali duniani ni kutoka kwa Mariela Shaker mkimbizi kutoka Syria aliyepata bahati ya kipekee ya kusoma kusoma katika chuo kikuu cha muziki cha Monmouth, Illinois Marekani.
Kama wasemavyo wahenga baada ya dhiki ni faraja, msemo ambao Mohamad, kijana barubaru kutoka Syria ambaye kwa sasa anaishi Uholanzi anaushuhudia, baada ya kuponea chupuchupu kujiunga na kikundi cha wanamgambo wa ISIL nchini Syria.
Nina wasiwasi na mapigano Kusini Magharibi mwa Syria ambapo raia wa kawaida ndio wamenaswa katika mapigano hayo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesihi Muungano wa Ulaya, EU, na wanachama wake kuchukua hatua thabiti, za pamoja na za wakati il kuokoa Maisha ya watoto wakimbizi na wahamiaji kabla hawajaingia barani Ulaya.