Baada ya kutoroka kusajiliwa ISIL sasa ndoto zangu zitatimia: Mohamad

9 Julai 2018

Kama wasemavyo wahenga baada ya dhiki ni faraja, msemo ambao Mohamad, kijana barubaru kutoka Syria ambaye kwa sasa anaishi Uholanzi anaushuhudia, baada ya kuponea chupuchupu kujiunga na kikundi cha wanamgambo wa ISIL nchini Syria.

Mohamad ambaye kwa sasa anaendelea na elimu katika mji wa Heerlen uliopo kusini-mashariki mwa Uholanzi,  anasimulia madhila aliyopitia nchini Syria wakati anakimbia vita sambamba na kuponea kusajiliwa na wanamgambo wa ISIL.
 

Nyumba yetu ilibomolewa pamoja na kumbukumbu nyingi za maisha. Siwezi kuijenga tena.”

Kama ilivyo kwa vijana wengi waliokimbia migogoro ya kivita Syria, Iraqi na Afghanistan , suala la kujiunga na kundi la wanamgambo wa ISIL lilikuwa sio hiari bali lazima.

Akiwa na miaka 14 wakati huo, Mohamad  alifanikiwa kutoroka usajili huo na kukimbia bila wazazi hadi Uholanzi ambako alifanikiwa kupewa hifadhi ya ukimbizi  miaka miwili iliyopita kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Na amekuwa na matumaini ya kuuganishwa na familia yake hapo baadaye.

Mohamad sasa ana umri wa miaka 16 akiishi peke yake bila mlezi katika nchi ya ugenini….

Nitajitahidi niweze kufanya kila kitu kwa kujitegemea mwenyewe. Nitajitahidi kufanya mwenyewe kila kitu maana sitegemei kutiwa moyo na mtu yeyote.”

Mohamad  anasema ana ndoto baada ya kumaliza shule….

Matarajio yangu ni kwamba nikimaliza shule ya sekondari, natamani kujiunda na chuo cha udaktari ili niwe mpasuaji, kwa sababu najua ukiwa mpasuaji maana yake ni kusaidia watu.”

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter