Nalaani vikali shambulio la kigaidi Sweida, huku ni kupuuza uhai wa watu:Guterres

26 Julai 2018

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea mjini Sweida Syria siku ya Jumatano.

Duru zinasema zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika milipuko kadhaa ya mabomu wakati wa shambulio hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Guterres amesema amesikitishwa na kughadhibishwa na shambulio hilo lililofanywa na kundi la kigaidi la ISIL ambalo limepuuza thamani ya uhai na maisha ya watu.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.

Pia ametoa wito wa kuhakikisha wote waliohusika na ukatili huo wanawajibishwa kisheria.

TAGS: Sweida, Syria, ISIL, ugaidi, Antonio Guterres

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter