Maafisa wenye mamlaka wamehusika na ukiukwaji wa haki Sudan Kusini - Ripoti
Ripoti ya tume ya Haki za Binadamu nchini Sudan Kusini iliyowasilishwa leo mijini Geneva Uswisi, imebaini kuwa watu 23 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita waliokuwa katika ngazi ya mamlaka nchini humo, wanakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu chini ya sheria za kimataifa kwa kutekeleza uhalifu mkubwa unaohusiana na vita nchini Sudan kusini.