Uwekezaji kwa vijana wakimbizi ni uwekezaji bora:Balozi Affey

22 Februari 2019

Kuwekeza kwa vijana wakimbizi walio kamimbini Kakuma nchini Kenya ni kuwekeza kwa amani na utulivu kwa kikanda . Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  kwa ajili ya Pembe ya Afrika, balozi Mohamed Affey baada ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Kakuma . 

 Balozi Affey akizungumza na vijana mbalimbali wakimbizi kambini hapo ,  ambao asilimia kubwa  ni kutoka Somalia na Sudan Kusini na baada ya kusikia maoni yao amesema anaamini uwekezaji kwa vijana hao utakuwa uwekezaji bora kwani
(SAUTI YA BALOZI  MOHAMED AFFEY)

“Nimefurahishwa sana na nilichokishuhudia Kakuma ambao ni mfano wa kimataifa wa jinsi wakimbizi na jamii za wenyeji wanavyoshirikiana, kufanya kazi pamoja na kusihi pamoja kwa utulivu.”

Picha/UN-Habitat/Julius Mwelu
Duka la kinyozi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kenya 2016

Asilimia kubwa ya vijana hawa wakimbizi wanakabiliwa na changamoto hasa za ajira na  kutimiza ndoto zao lakini Balozi Affey anasema hawajakata tamaa 

(SAUTI BALOZI  MOHAMED AFFEY)

Nimehamasishwa na niliyoyashuhudia , mnepo na matumaini machoni mwa wakimbizi  hawa licha ya changamoto zinazowakabili kila siku, nimetiwa moyo na wasichana niliowaona katika shule za msingi za Morneau Shappelle na Anjelina Jollie ambao wanatutia matumaini kwamba, mustakabali wa ukanda wetu utadhibitiwa na jinsi tunavyowahudumia na kuwapa elimu, na ni ishara kwamba tukiwekeza kwa vijana hususan kwa vijana wakimbizi tunawekeza kwa amani na utulivu wa kikanda.”

UNHCR imekuwa msitari wa mbele kwa kushirikiana na wadau wengine kuwekeza katika miradi mbalimbali itakayohakikisha vijana wakimbizi wanakuwa na matumaini ya maisha na mustakbali wao.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud