Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaanzisha kampeni ya chanjo dhidi ya surua, Sudan Kusini

Mama na mwana wapewa chanjo. Chanjo nyingi hutokea baada ya milipuko ya magonjwa  kama vile Polio, Kipindupindu na magonjwa mengine.
UNICEF/ Nangyo
Mama na mwana wapewa chanjo. Chanjo nyingi hutokea baada ya milipuko ya magonjwa kama vile Polio, Kipindupindu na magonjwa mengine.

UN yaanzisha kampeni ya chanjo dhidi ya surua, Sudan Kusini

Msaada wa Kibinadamu

Kampeni kubwa ya kutoa chanjo kwa ziadi ya watoto 40,000 dhidi ya surua imezinduliwa leo katika eneo la Mayom iliyokuwa ikijulikana kama jimbo la Unity nchini Sudan Kusini..

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja, kampeni hiyo inaendeshwa na wizara ya afya ya Sudan Kusini kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na shirika la afya ulimwenguni, WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM wakati huu ambapo kumeripotiwa mlipuko katika kaunti ya Mayom.

Takriban visa 17 bila vifo vyovyote vimeripotiwa katika kaunti ya Mayom huku karibu asilimia 90 ya waathirika ni watoto wa chini ya umri wa miaka mitano wakitoka maeneo ya Pup na Mankien Payams.

Kampeni hiyo ya siku tisa itakayokamilika tarehe 14 mwezi huu wa Machi inalenga watoto 37, 193 walio na kati  ya umri wa miezi sita hadi miaka minne na nusu katika maeneo 10  ambayo ni Kuerbona, Mankien, Riak, Ruathnyibol, Kueryiek, Ngop, Pub, Bieh, Wangbour and Wangkei.

Surua ni ugonjwa unaoambukiza sana na unasababisha ubongo kuvimba, kuhara, homa ya kichomi na upofu. Taarifa ya mashirika hayo imesema watoto wachanga walio na utapiamlo na kinga duni ya mwili wako hatarini kuumua na hata kufa. Hatahivyo surua ina kinga kwa kupokea chanjo ambayo ni salama.

Surua nchini Sudan Kusini inatokana na idadi kubwa ya watoto ambao hawajapokea chanjo ikiwa ni asilimia 59. Aidha upatikanaji wa huduma ya afya kote nchini ni chini ya asilimia 50 ya watua mabo wanakadiriwa kuishi kilometa tano karibu na kituo cha afya. Kama njia ya kukabiliana na surua, kampeni zinazolenga watoto hufanyika kila miaka miwili.

Kampeni ya mwisho kufanyika ilikuwa mwezi Mei mwaka  2017 ambapo ifilikia watoto zaidi ya milioni 1.9 ya watoto 2.3 walengwa wa umri kati ya miezi tisa na chini ya miaka mitano.

Yaelezwa kuwa baadhi ya kaunti hazikufikiwa kwa ajili ya ukosefu wa usalama. Kampeni nyingine ya nchi nzima imelengwa kufanyika baadaye mwaka huu na kupunguza idadi ya watoto waliohatarini kuambukizwa na ambao hawajachanjwa, na hivyo kupunguza hatari ya maambukizi zaidi.