Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Uganda, vinara wa kuwalinda Sokwe wasitoweke.

Wanawake Uganda, vinara wa kuwalinda Sokwe wasitoweke.

Pakua

Kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha binadamu kusogea zaidi katika makazi asili ya wanyama, mara kadhaa binadamu na wanyama wameingia katika mgogoro ambao unaziathiri pande zote mbili. Migogoro hiyo ni pamoja na wanyama kuvamia makazi ya binadamu na hata kuharibu mashamba huku binadamu nao wakisambaratisha makazi ya wanyama.

Nchini Uganda, shirika moja lisilo la kiserikali limewaelimisha wanawake wa kijiji cha Wagaisabi wilayani Hoima kuhusu malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs ambapo miongoni mwa mafunzo waliyoyapata ni pamoja na kuyatunza mazingira ya asili ili kuwalinda Sokwe. John Kibego amewatembelea wanawake hao ambapo ametuandalia makala ifuatayo.

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UNEP