Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde wanachama hizi ndio hatua tunazopaswa kuchukua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN

Watu wanaoishi katika visiwa vya Comoro kwenye bahari ya Hindi wanahitajhi kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
UNDP Comoros/James Stapley
Watu wanaoishi katika visiwa vya Comoro kwenye bahari ya Hindi wanahitajhi kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Chonde chonde wanachama hizi ndio hatua tunazopaswa kuchukua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN

Tabianchi na mazingira

Kabla ya mkutano wa kimataifa wa mabadilkiko ya tabianchi ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Giuterres mwezi Septemba mwaka huu, leo Umoja wa Mataifa na mashirika yake wameafikiana hatua madhubuti za kuchukua.

Maafisa hao wa kimataifa pia wamesisitiza ahadi ya kukidhi mahitaji ya nchi wanachama ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kukabiliana na matokeo ya majanga.

Maafikiano hayo yamefanyika leo mjini Geneva Uswis wakati wa mkutano wa majira ya chipukizi wa bodi ya wakurugenzi ya Umoja wa mataifa (CEB) , ambako wamesisitiza ahadi zao za kuimarisha mashirika yao katika kushughulikia mahitaji ya nchi wanachama , kuzijengea mnepo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha hatua zao katika mifumo ya ulinzi wa kijamii kwa ajili ya matukio yanayohusiana na masuala ya tabianchi.

 

Familia huko nchini Burkina Faso ikienda kusaka maji. Nchini humo zaidi ya watu 950,000 hawana uhakika wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ukame na hivyo kukwamisha shughuli za kilimo na ufugaji.
OCHA/Otto Bakano
Familia huko nchini Burkina Faso ikienda kusaka maji. Nchini humo zaidi ya watu 950,000 hawana uhakika wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ukame na hivyo kukwamisha shughuli za kilimo na ufugaji.

Wito kwa nchi wanachama

“Sisi viongozi wa mfumo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa tunatoa wito kwa nchi wanachana kuendeleza azma na kuchukua hatua halisi za kupunguza kiwango cha joto la dunia hadi  nyuzi joto 1.5 ° C juu ya viwango vya kabla ya mapinduzi ya viwanda na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kama ambavyo wanajitahidi kutimiza majukumu yao ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya afya, haki ya uhakika wa chakula, haki ya maendeleo, haki za watu wa asili, jamii za mashinani, wahamiaji, watoto, watu wenye ulemavu na watu walio katika mazingira magumu, pamoja na usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, usawa wa kizazi hiki, na ajira bora na mabadiliko ya haki kwa wote, kama ilivyoelezwa katika Mkataba wa Paris. Kama ilivyoelezwa na ripoti maalum ya IPCC kuhusu ongezeko la  joto duniani, kuhakikisha tunadhibiti joto hilo na inasalia nyuzi joto 1.5 ° C ni muhimu ili kuzuia mabadiliko yasiyotarajiwa. Kufikia lengo hili itahitaji mabadiliko kwa kiwango kikubwa kabisa katika ngazi zote, lakini bado inawezekana ikiwa tutatenda na kuchukua hatua sasa. Kwa haraka sana tunatoa wito kwa nchi wanachama wa Mataifa kuja New York mwezi Septemba na mawazo, na mipango madhubuti ya kuongeza michango yao ya kitaifa ya maamuzi ya 2020 na kuunga mkono utekelezaji wa Malengo ya maendeleo endelevu SDGs.”

Ripoti ya karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu bayoanuai imeonyesha kwamba athari zintokanazo na shughuli za binadamu kwenye mazingira zinatishia karibu viumbe milioni moja kwa miongo kadhaa, huku juhudi za sasa za kulinda rasilimali za nchi kavu huenda zikashindwa endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa.

Mtazamo wa bahari ambayo inabeba raslimali nyingi.
UN News/ Anton Uspensky
Mtazamo wa bahari ambayo inabeba raslimali nyingi.

Mnepo

Viongozi hao wametoa wito kwa nchi wanachama kuhakikisha kwamba hatua za kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zinachukuliwa ili kulinda watu, maisha yao na mfumo mzima wa maisha hususan watu walio katika kanda ambazo ziko hatarini zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo walio katika hatari kupitia kulazimika kukimbia na uhamiaji.

Wamezitaka nchi wanachama kubaini na kujenga uwezo na suluhu katika jamii zilizo hatarini, mifumo, kuweka rasilimali za kutosha , kusaidia mchakato wa kubaini uchumi, masuala ya kijamii na haki za kitamaduni kwa watu wote , ili kuhakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma.

Mfumo wa Umoja wa Mataifa unazisaidia nchi wanachama kusaka njia jumuishi , zisizo na hatari za maendeleo endelevu na kuimarisha hatua ufuatiliaji, kuzuia na kudhibiti hali ya hewa na hatari za majanga, ikiwemo kupitia kuchagiza mipango ya kitaifa ya mnepo na maendeleokwenye masuala ya mikakati ya kitaifa ya upunguzaji majanga.

Ufadhili

Ufadhili wa masuala ya tabianchi ni muhimu sana katika utekelezaji wa hatua katika kiwangi kinachotakiwa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Katika suala hilo la kukusanya fedha nchi zilizoendelea kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni lazima zitimize lengo la kuchangisha fedha kwa kuzichagiza serikali na sekta binafsi kuhakikisha zinafikia lengo la dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2010 kuweza kusaidia hatua za mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi zinazoendelea na kuimarisha zaidi juhudi zao za kuchagisha feza kwa ajili ya mapambano hayo.