Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya asili ya wafugaji inasaidia mnepo wa mabadiliko ya tabianchi:TANIPE

Teknolojia ya asili ya wafugaji inasaidia mnepo wa mabadiliko ya tabianchi:TANIPE

Pakua

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hazichagui wala hazibagui taifa au jamii utokayo zinamuathiri kila mtu duniani na ndio maana wito unatolewa kila uchao kuchukua hatua zote stahiki kujenga mnepo dhidi ya zahma hiyo kote duniani. Wito huo hivi sasa unaitikiwa sio tu na serikali mbalimbali kuweka será na mikakati , bali pia wadau wote wakiwemo asasi za kiraia ,sekta binafsi, jamii na hata mashirika ya kijamii. Miongoni mwa wadau hao ni shirika lisilo la kiserikali la TANIPE nchini Tanzania lenye makao yake makuu mkoani Morogoro, ambalo linajikita zaidi na wafugaji wa asili kama Wamaasai nchini humo ili kuwajengea uwezo na kuboresha teknolojia zao za asili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Katika makala hii mkurugenzi mkuu wa TANIPE Edward Tunyon amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa jukwaa la Umoja wa Mataifa la watu wa asili linaloendelea mjini New York Marekani  kuhusu wanavyowasaidia jamii hizo za wafugaji kuwa na mnepo. Edward anaanza kwa kufafanua wafugaji wa asili ni wapi

 

 

Audio Credit
Patrick Newman/ Flora Nducha/ Edward Tunyon
Audio Duration
5'15"
Photo Credit
UN News Kiswhaili/Patrick Newman