Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimejifunza watu wenye Down Syndrome wanaweza kuishi maisha ya kawaida wakijumuishwa – Elly Kitaly

Nimejifunza watu wenye Down Syndrome wanaweza kuishi maisha ya kawaida wakijumuishwa – Elly Kitaly

Pakua

Hivi karibuni katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefanyika mkutano wa Siku ya Kimataifa ya Down Syndrome. Mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu “Pamoja nasi, kwa ajili yetu” uliandaliwa na taasisi ya Down Syndrome International (DSI) kwa kushirikiana na taasisi ya The International Disability Alliance (IDA), Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa wa Brazil, Japan na Poland.  

Mmoja wa waliohudhuria mkutano huo ni Elly Kitaly, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa asasi ya kijamii iitwayo Chadron’s Hope Foundation inayohusika na kujenga mazingira bora kwa watu wenye hali ya Down Syndrome nchini Tanzania anaeleza aliyojifunza katika mkutao huo.  

Audio Credit
Selina Jerobon/Anold Kayanda
Audio Duration
3'14"
Photo Credit
Chadron's Hope Foundation/Elly Kitally