Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utiaji alama silaha utafanikisha amani na usalama mashariki mwa DRC

Utiaji alama silaha utafanikisha amani na usalama mashariki mwa DRC

Pakua

Mashambulizi dhidi ya raia yanayoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yanachochewa pia na kitendo cha makundi ya waasi kumiliki silaha. Silaha zinaripotiwa kupatikana kiholela na kutishia usalama wa rai ana mali zao. Ni kwa kutambua hilo, hivi karibuni ofisi ya  Umoja wa Mataifa ya huduma ya kutegua mabomu UNMAS kwa ushirikiano na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, DRC MONUSCO waliendesha operesheni ya wiki mbili ya kutia alama kwenye silaha lengo likiwa ni kuhakikisha usimamizi bora wa silaha hizo. Je nini kilifanyika? George Musubao, mwadishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC alikuwa shuhuda wetu na ametuma makala hii.

Audio Credit
Anold Kayanda/George Musubao
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UN News/George Musubao