Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za utupaji wa taka za plastiki kwenye maziwa na baharí

Athari za utupaji wa taka za plastiki kwenye maziwa na baharí

Pakua

Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya bahari unatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na baadhi ya taka ikiwemo plastiki kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa viumbe hao.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukizitaka nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti taka hizo katika mataifa yao ili kuokoa Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji pamoja na mfumo wa Ikolojia.

Kutoka jijini Mwanza kaskazini-magharibi mwa Tanzania, Evarist Mapesa alikutana na Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Sayansi wa Maji na Mazingira yake na Teknolojia za Uvuvi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Bahati Mayoma, akitaka kufahamu athari za taka za plastiki kwa viumbe hai waishio kwenye maji na hapa mhadhiri huyo anaeleza.

Audio Credit
Selina Jerobon/Evarist Mapesa
Audio Duration
3'5"
Photo Credit
UN News