Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuhamasishe mawazo chanya duniani – Mchechemuzi wa SDGs, Chioma Ogbonna “Cill”

Tuhamasishe mawazo chanya duniani – Mchechemuzi wa SDGs, Chioma Ogbonna “Cill”

Pakua

Mwanamuziki wa Nigeria Chioma Ogbonna akifahamika kwa jina la usanii “Cill” ni mchechemuzi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG Action Campaign ambaye hivi karibuni alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zenye maendeleo duni Duniani, LDC5.  

Moja ya nyimbo zake maarufu ni Woman alioutoa mwaka 2021 ukiwa mahususi kwa ajili ya Siku ya Mwanamke Duniani. Ni wimbo ambao unaeleza nguvu ya mwanamke licha ya kukatishwa tamaa. Nyimbo zake nyingine maarufu za Cill ni pamoja na Tatarata, Kachifo, Permit me na nyinginezo kadhaa.  

Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na msanii huyu mjini Doha nchini Qatar. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Anold Kayanda
Audio Duration
4'46"
Photo Credit
UN News/Anold Kayanda