Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakikisho la maji safi na salama lachochea jamii kuishi na utangamano Mkoani Kigoma nchini Tanzania

Hakikisho la maji safi na salama lachochea jamii kuishi na utangamano Mkoani Kigoma nchini Tanzania

Pakua

Ufumbuzi wa ubunifu wa maji unaotumia teknolojia ya nishati ya jua ambao unafanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wake ukiwemo ule wa utekelezaji, Water Mission, na ule wa kutoa msaada wa fedha Grundfos Foundation kutoka nchini Denmark umesaidia serikali ya Tanzania kubuni suluhisho la msingi na la kudumu la maji katika jamii 15 za mkoa wa Kigoma ulioko magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Lengo lao kubwa ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa watu 99,107 mkoani humo ifikapo Machi 2024. 

Miongoni mwa wanufaika ni jamii, wanafunzi na wahudumu wa afya katika hospitali, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikumbwa na changamoto za ukosefu wa maji na migogoro kati yao inayotokea mara kwa mara wakati kundi kubwa la watu linapokutana katika mto moja ulioko mbali kuteka maji. Hali ilikuwa vipi kabla na baaannoda ya mradi huo? Ungana basi na Selina Jerobon katika makala hii iliyofanikishwa na UNICEF. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Selina Jerobon
Audio Duration
5'48"
Photo Credit
UNICEF