Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNDP/Sawiche Wamunza

Matunda ya ubia katika kuhifadhi wanyamapori wazaa matunda pori la Waga Tanzania

Nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa Jumuiya za Hifadhi za WAnyamapori, WMAs, unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii nchini humo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP wa kuzuia ujangili na uhifadhi wa wanyamapori umesaidia jamii kunufaika sio tu na uwepo wa wanyamapori kwenye maeneo yao lakini pia kuishi kwa utangamano na wanyama kwa kuzingatia kuwa leo ni siku ya wanyamapori duniani na ujumbe ni ushirikishaji jamii katika hifadhi ya wanyamapori.

Sauti
5'35"
UNDP Guatemala/Caroline Trutmann

Baada ya hofu kubwa ya soko Peru, IFAD yaleta matumaini makubwa

Miaka miwili iliyopita, wakulima nchini Peru walikuwa na hofu ya kwamba janga la COVID-19 lingalifuta kabisa masoko yao waliyozoea kuuza mazao kama vile kakao na malimao. Walizoea kuuza sokoni lakini COVID-19 ilifuta masoko hayo kutokana na vizuizi vya kutembea.

Hata hivyo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD kupitia mradi wa kuchechemua kilimo vijijini baada ya COVID-19 ulileta nuru na sasa wakulima hawaamini kile wakipatacho. Ni kwa vipi basi? Ungana na Assumpta kwenye makala hii iliyoandaliwa na IFAD. 

Sauti
3'9"
© MINUSCA

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wametufundisha kutumia majembe – Wakulima CAR

Wananchi wa Kijiji cha Difolo katika viunga vya mji wa Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamewashukuru walinda amani wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MINUSCA) baada ya wanalinda amani hao kuwafundisha wananchi hao kulima kwa kutumia jembe la mkono badala ya kulima kwa kutumia panga. Kapteni Mwijage Francis Inyoma ni Afisa Habari wa kikosi hicho ameandaa makala hii. 

Sauti
4'16"
© UNDP/Oleksandr Ratushniak

Mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi Ukraine, UN yataka vita ikome 

Hii leo ni mwaka mmoja tangu Urusi ivamie Ukraine! Ndani ya mwaka mmoja wa uvamizi huo, zaidi ya watu 8,000,000 wamekimbia nchi hiyo, zaidi ya 5,000,000 ni wakimbizi wa ndani ilhali theluthi moja ya wananchi wote hawako kwenye makazi yao. Watu milioni 17.6 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu ambapo zaidi ya milioni 16 wameshafikiwa na msaada muhimu. Nini kimetokea katika mwaka huo mmoja? Umoja wa Mataifa umechukua hatua gani kufikia wahitaji? Assumpta Massoi anasimulia katika makala hii. 

 

Sauti
6'30"
UN News

Kulima tunalima lakini lishe bado ni changamoto tuchukue hatua- Mkulima Sarah

Jamii ya mikunde! Wengi wanaitambua zaidi kama ni kunde zenyewe, na maharagwe lakini ni zaidi ya hiyo. Kuna choroko, mbaazi, dengu, njegere na kadha wa kadha ambapo kutokana na umuhimu wake katika lishe ya binadamu, kurutubisha udongo na pia kuhimili mabadiliko ya tabianchi, ndio maana Umoja wa Mataifa unapigia chepuo.

Mathalani nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO linafadhili mradi wa AgriConnect ambao pamoja na mambo mengine  unapatia wananchi, wake kwa waume stadi za mapishi sahihi ya jamii ya mikunde.

Sauti
4'55"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Harakati za Hope for Girls and Women in Tanzania kupigania haki za kijamii nchini Tanzania

Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa Haki ya kijamii inafanya jamii na uchumi wa jamii hizo kufanya kazi vizuri na kupunguza umaskini, ukosefu wa usawa na mivutano ya kijamii. Haki ya Kijamii ina jukumu muhimu katika kufikia njia shirikishi zaidi na endelevu za maendeleo ya kijamii na kiuchumi na ni muhimu kwa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ndio maana Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau na kila mtu kushiriki katika kuhakikisha haki za kijamii zinalindwa.

Sauti
3'50"
© UNHCR/Samuel Otieno

UNHCR na usaidizi kwa wakimbizi wa Burundi waliorejea nyumbani

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaendelea na hatua zake za kuhakikisha wakimbizi waliorejea nyumbani wanaishi maisha ya utu na ustawi, ambapo pamoja na kuwapatia wakimbizi hao huduma bora pia linazidi kuomba wahisani waoneshe ukarimu zaidi.

Tuungane na Edouige Emuresenge wa Televisheni washirika, Mashariki TV nchini Burundi katika makala hii iliyoandaliwa na UNHCR. 

Sauti
3'
UN News/Byobe Malenga

Redio Ngoma ya Amani inachangia utunzaji wa amani hapa mashariki mwa DRC - Wasikilizaji

Katika Siku ya Redio Duniani mwaka huu wa 2023, UNESCO inaangazia redio huru kama nguzo ya kujenga amani na kuzuia migogoro. 

Redio inatazamwa kama chombo muhimu na sehemu muhimu ya kutunza amani. Redio hushughulikia visababishi na vichochezi vya migogoro, kabla hazijaweza kulipuka na kuwa vurugu. Inatoa mbinu mbadala ya kuzuia migogoro, au migongano ya maslahi, kuondoa kutoelewana, na kutambua masuala ya kutoaminiana. Hii inaweza kusaidia kukabiliana na chuki, hamu ya kulipiza kisasi, au nia ya kutumia silaha. 

Sauti
4'25"