Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde UN tusaidie tujue ukweli kuhusu mauaji ya jamaa zetu- Mkazi Beni, DRC

Chonde chonde UN tusaidie tujue ukweli kuhusu mauaji ya jamaa zetu- Mkazi Beni, DRC

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mashambulizi yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo kwenye jimbo la Kivu Kaskazini yanasababisha sio tu vifo bali machungu yasiyoisha kwa familia za waliouawa kwa kushindwa kufahamu ukweli wa nini kiliwafika jamaa zao, nani aliwaua, na haki gani imetendeka na sheria dhidi ya waliohusika. 

Hii leo katika makala na ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki ya kupata ukweli kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utu kwa waathirika mwandishi wetu nchini DRC, George Musubao amefunga safari hadi kwenye makazi ya mmoja wa waliopoteza jamaa zao na kufahamu hali iko vipi na zaidi ya yote Umoja wa Mataifa unafanya nini. 

Audio Credit
Selina Jerobon/George Musubao
Audio Duration
4'16"
Photo Credit
MONUSCO/George Musubao