Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana wa kiume apazia hatua dhidi ya ukeketaji nchini Kenya

Kijana wa kiume apazia hatua dhidi ya ukeketaji nchini Kenya

Pakua

Mila potofu ya ukeketaji watoto wa kike na wanawake bado imeendelea kujikita katika jamii mbalimbali duniani licha ya nuru kuonekana katika baadhi ya maeneo kuwa ukeketaji unaanza kufifia. Umoja wa Mataifa unasema kuwa mwaka 2019 wasichana milioni 4.1 walikuwa hatarini kukeketwa na kutokana na makadirio ya ongezeko la idadi ya watu, idadi hiyo inaweza kufikia milioni 4.6 mwaka 2030. Ni kwa mantiki hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA linasaka ushirikiano na wadau mashinani ili kuondokana na mila hiyo potofu, wito ambao umeitiwa na vijana kama vile Vincent Mwita kutoka kaunti ya Migoro nchini Kenya. Katika mahojiano na mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi, Vincent mwenye umri wa miaka 28 kutoka kabila la wakurya anaanza kuelezea kile anachofanya.

Audio Credit
Assumpta massoi/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania