Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunataka kubadilisha mtazamo wa watu warejee katika vyakula vya kienyeji - Miriam Nabakwe

Tunataka kubadilisha mtazamo wa watu warejee katika vyakula vya kienyeji - Miriam Nabakwe

Pakua

Umoja wa Mataifa uliutangaza mwaka huu wa 2021 unaoelekea ukingoni kuwa mwaka wa mbogamboga na matunda lengo likiwa ni kuelimisha watu kuhusu umuhimu na faida za mbogambona na matunda mwilini. Miriam Nabakwe wa nchini Kenya anasema tatizo hilo la watu kutokula mbogamboga lipo na mbaya zaidi ni kuwa hata vyakula ambavyo watu sasa wanavithamini si vile vya asili na hivyo kuongeza tatizo juu ya tatizo kwani anaamini vyakula vya asili vilivyosalia katika maeneo mbalimbali duniani ndivyo vyenye virutubisho asilia. Kwa msingi huo ameamua kufanya juhudi binafsi kuwahamasisha watu wa nchini mwake Kenya angalau kwa kuanzia katika mji mkuu, Nairobi ili watu warejee katika ulaji wa vyakula vya asili. Anafanyaje? Tuungane na mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi ambaye amezungumza naye. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'34"
Photo Credit
© FAO-Magnum Photos/Alex Webb