Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

World Bank/Flore de Preneuf

Kijana mwanamazingira Rebecca Laibich ajitolea kufundisha wengine

Katika makala hii leo tunajiunga na mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi akizungumza na Rebecca Laibich, kijana mwenye umri wa miaka 25 mwanaharakati wa kuhifadhi mazingira nchini Kenya na mfanyakazi wa kujitolea wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, ambaye amejitwika jukumu la kuwafunza vijana wenzie kuhusu umuhimu na njia za kutunza mazingira.

Sauti
3'20"
UNMISS/Eric Kanalstein

Kupitia asali nimeweza kuwapatia wanawake na vijana shughuli ya kipato

Msichana Joreen Wanini wa nchini Kenya, mfanyabiashara ya asali ambaye amefikia hatua ya kuwa chanzo cha ajira kwa watu wengine hususani wanawake na vijana, anawaambia vijana wenzake wawekeze kwenye kilimo na mazao ya kilimo kwani mara zote watu watahitaji chakula na itakuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi katika jamii.

Joreen alijiajiri mara tu baada ya kumaliza masomo yake akinunua asali kutoka kwa wakulima wadogowadogo na kuiongezea thamani kwa kuiweka katika vifungashio vizuri kisha kuuza kwa watu wengine wenye uhitaji hasa katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.

Sauti
3'46"
© World Bank/Arne Hoel

Mradi wa ufugaji wa sungura na kuku wae ndelea kutumika kupamba na udumavu Tanzania

Lishe duni kote duniani ni tishio kubwa kwa ustawi wa binadamu kutokana na uhaba wa chakula kwa upande mmoja, na wakati mwingine ukosefu tu wa elimu kuhusu matumizi bora ya vyakula vinavyopatikana katrika jamii. Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs, kwa namna tofauti tofauti yanalenga pamoja na mambo mengine, kuliondoa tatizo hili ili kuwaokoa afya za watu hususani watoto duniani kote.

Sauti
3'27"
John Kibego

Uganda yaimarisha utoaji chanjo dhidi ya COVID-19

Serikali ya Uganda imeamua kushirikiana zaidi na wadau mbalimbali ikiwemo makampuni ya mawasilaino na yale ya vinywaji katika juhudi za kuimarisha chanjo dhidi ya COVID-19.

Kampuni ya bia ya Nile Breweries imelivalia njuga suala la kuhamasisha wateja wake kupata chanjo hiyo itakayotegemewa na serikali ili kufungua sekta yao iliyofungwa tangu mwaka jana na zingine. Je, kampeni hiyo inatekelezwaje? Na mtazamo wa raia wa Uganda kuhusu chanjo huyo ukoje sasa?

Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego anaripoti.

 

Sauti
3'52"
UN/ John Kibego

Jamii ya Watyaba kandoni mwa Ziwa Albert nchini Uganda yatishiwa tena na mafuriko

Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 unaendelea katika huko Glosgow na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa amewaeleza viongozi wa ulimwengu kuwa ni muhimu kuchukua hatua sasa kwani wanadamu wanajichimbia kaburi, nchini Uganda jamii ya Watyaba, mojawapo ya jamii za walio wachache wanaoishi katika viunga vya Ziwa Albert, wanapaza sauti kwa serikali na shirIka  la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kuwasaidia kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
3'45"