Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaani hakuna kazi lakini kuna fursa tutumie tujikwamue – Dorcas 

Mtaani hakuna kazi lakini kuna fursa tutumie tujikwamue – Dorcas 

Pakua

Kijana Dorcas Mwachia anakaribia kuhitimu shahada ya uzamili huko nchini Kenya. Ingawa hivyo katika kuelekea kutamatisha safari yake amegundua kuwa hana uwezo kifedha wa kumalizia karo na njia pekee ni kubonga bongo ajikwamue yeye na nduguye. Pitapita ya mitaa ya Nairobi nchini Kenya ikamkutanisha na chupa zilizotumika ambazo kwake yeye akaona ni fursa, huku akisafisha mazingira na wakati huo huo anazitumia kutengeneza mapambo anayouza. Kipato mfukoni na mazingira yanakuwa safi na sasa ameweza kukamilisha karo ya Chuo Kikuu na mengine mengi. Ungana na Jason Nyakundi mwandishi wetu wa Kenya ambaye amezungumza na Dorcas akianza kuelezea safari yake. 

Audio Credit
UN News/Jason Nyakundi-stringer
Sauti
3'8"
Photo Credit
UN/ Jason Nyakundi