Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

World Bank/Sambrian Mbaabu

Niliyaishi maisha ya kurandaranda mitaani, ninafahamu wanachokipitia. 

Tangu umri wa takriban miaka 6 Joseph Njoroge Wanyoike aliishia kuwa mtoto wa kurandaranda mitaani mjini Nairobi. Kutokana na mkono wa msamaria mwema, Joseph amefanikiwa katika maisha na sasa ameamua naye kurejesha kwa jamii. Kwa sasa Joseph Njoroge anamiliki kituo cha kuwatunza na kukuza vipaji  vya vijana wa kurandaranda mitaani vikiwemo vya kucheza soka katika mji mdogo wa Ngong’ nje ya mji wa Nairobi.  Mwandishi wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza naye kutaka kufahamu safari yake

Sauti
3'37"
Doris Mollel Foundation.

Aweka faida kando kuunga mkono hoja ya UN ya afya kwa kila mtu

Afya bora ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa.

Mara nyingi mtu akianzisha biashara, mathalani ya kutoa huduma za hospitali, lengo huwa ni kutafuta faida na kujiendeleza na ni wachache mno wanaotumia biashara zao kunufaisha jamii bila malipo.

Florence Kabii ni miongoni mwa wachache hao ambao biashara yake ya hospitali imekuwa tumaini na kimbilio la wengi wasiojiweza katika eneo la Molo, kaunti ya Nakuru nchini Kenya.

Sauti
4'36"
UN News/ John Kibego

Mienendo ya ujanani inavyoweza kuwa baraka au balaa uzeeni -Sehemu ya kwanza

Mienendo ya mtu katika ujana wake hutoa matunda yake au machungu wakati wa uzee, anasema mzee mmoja nchini Uganda aitwaye Peter Semiga ambaye sasa ametimiza umri wa miaka 80. 

Mienendo hiyo ambayo kulingana na uzoefu wake ni hatari kwa mustakbali wa kijana ni pamoja na tabia mbaya ya matumizi ya pesa, uvutaji wa sigara, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo vingine. 

Sauti
3'31"
UN

Waganda wapaza sauti baada ya intaneti kurejeshwa

Nchini Uganda kuelekea uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wiki iliyopita, mamlaka ziliamuru kuzimwa kwa mtandao wa intaneti na  baadaye huduma hiyo ilirejeshwa tarehe 18 mwezi huu wa Januari na matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Baadhi ya wananchi walikuwa na mtazamo tofauti kuhusu hatua hiyo ambapo mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego alivinjari kuzungumza nao kufahamu mitizamo hiyo baada ya huduma kurejea na ndipo akaandaa makala hii.
 

Sauti
2'42"
UNIC/Ahimidiwe Olotu

Tuzo za kimataifa za  lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert kutolewa kesho Tanzania

Nchini Tanzania kesho Jumatano kunatolewa tuzo na nishani za kimataifa za lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert. Tukio hilo litafanyika kwenye mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Dodoma, ambapo tukio linaleta pamoja washiriki na manguli na wabobezi wa lugha ya Kiswahili kutoka maeneo mbalimbali duniani, na litahusisha pia viongozi waandamizi wa serikali na mashirika ya kitaifa na kimataifa. Lakini tuzo hizo zilianzia wapi? Na ni nini mantiki yake?

Sauti
6'
© UNICEF/UNI342042/

Janga la COVID-19 halikumzuia mzazi Ghana kuhakikisha watoto wanaendelea kujifunza

Nchini Ghana, janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 lililoibuka mwezi Machi mwaka jana wa 2020 lilitikisa shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mathalani shule zilifungwa na hivyo kutikisa pia ari ya wazazi waliokuwa wakijitolea kufundisha hasa katika shule zilizoko vijijini. Mwelekeo wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan namba 4 kuhusu elimu bora ulikuwa mashakani. Wazazi walishajitolea kusaidia maeneo ya vijijini lakini kufungwa kwa shule kukaleta hofu.

Sauti
3'31"
UN Women/Müslüm Bayburs

Hellen Obiri, mwanajeshi kutoka jeshi la anga la Kenya anayetamba duniani kwa mbio 

Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa michezo ina uwezo wa kubadili dunia, ni haki ya msingi, nyenzo muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, amani, mshikamano na kuheshimiana na ndio maana katika makala ya leo tunamwangazia Hellen Obiri mwanariadha kutoka jeshi la anga la Kenya bingwa wa dunia mbio za mita 5,000.  Obiri alizaliwa huko Kisii magharibi mwa Kenya lakini kwa jitihada zake amefanikiwa kufikia kiwango cha mwanariadha wa kimataifa anayesifika.

Sauti
3'44"
© FAO/IFAD/WFP/Petterik Wiggers

Ili kutokomeza njaa Tanzania tunapambana na mizizi ya tatizo hilo:WFP 

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limesema njaa ni tatizo mtambuka ambalo linachangia nchi nyingi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Na ili kutimiza malengo hayo nchini Tanzania WFP imeweka mkakati wa miaka mitano kushughulikias maeneo matano ambayo ni mizizi ya tatizo hilo ili kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 ukomo wa utekelezaji wa SDGs lengo namba 2 la kutokomeza njaa linatimia pamoja na malengo mengine. Je ni maeneo gani hayo? Tuungane na Ahimidiwe Olotu wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania. 

Sauti
4'35"
UN Women /Aidah Nanyonjo

Wasichana wapata stadi za kuwasaidia kustawi licha ya  COVID-19 na mafuriko nchini Uganda

Mafuriko ya mara kwa mara makazi hasa katika maeneo ya ziwa Albert nchini Uganda sambamba na athari za COVID-19 yameathiri ustawi wa watu katika matabaka mbalimbali. Vijana hasa wa kike wanaripotiwa kuingia katika hatari za kubakwa, na kutumbukia kwenye ndoa za utotoni na madhara yake. Kikundi cha Kaiso Women’s Group kwenye Ziwa Alebrt wilayani Hoima wanajitahidi kupambana na hali hiyo kwa kuwsafunza baadhi ya wasichana pamoja na wanawake ufundi cherehani na utengenezaji wa sabuni miongoni mwa mengine ambayo tayari vimeleta nuru.

Sauti
3'38"