Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNFPA/Luis Tato

UNFPA na Taasisi ya Panzi DRC yaingia makubaliano kunusuru manusura wa ukatili wa kingono 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamekuwa mwiba siyo tu katika usalama wa taifa hilo bali pia kwa wanawake na wasichana ambao hukumbwa na ukatili wa kingono kule kwenye mapigano. Mashirika ya kiraia yamekuwa yakiunga mkono harakati za Umoja wa Mataifa za kuhakikisha manusura wa ukatili huo wanarejeshewa siyo tu utu lakini pia kujiamini na kuendelea na maisha. Miongoni mwa mashirika hayo ni taasisi ya hospitali ya Panzi inayoongozwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dokta Denis Mukwege.

Sauti
4'57"
Delight Uganda Limited

Tuzo ya UNCTAD imenipa motisha zaidi kusaidia jamii – Dkt Julian Omalla

Mshindi wa tuzo ya wanawake wajasiriamali iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD na pia akapigwa jeki ya mkopo nafuu wa dola milioni 10 kutoka kwa serikali ya Uganda ameeleza alivyopokea tuzo hiyo na mipango ya baadaye. Akizungumza na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego, Dkt Julian Omalla ambaye amejipatia umaarufu kutokana na shughuli za kujikwamua pamoja na maelfu ya wanawake na vijana, amesema amepata maono makubwa zaidi baada ya kutunikiwa tuzo.

Sauti
3'42"
Pete Muller for the ICC

Mradi wa UN Women wa haki za ardhi za wanawake wakaribishwa, Uganda

Mradi wa UN Women wa kuimarisha ulinzi wa haki za ardhi za wanawake umeleta matumaini makubwa ya kupiga jeki juhudi za serikali kupambana na vikwazo vya kimila vinavyowakera wanawake nchini Uganda.

Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego baada ya kuzungumza na wadau kadhaa wa masuala ya jinsia na maendeleo kuhusu mradi huo unaotekelezwa na shirika la kiraia la Mid-western Anti-corruption Coalition, MIRAC, ametuandalia makala ifuatayo.

Sauti
3'33"
UNEP/Duncan Moore

Wanawake wa Pwani ya Kenya kusikilizwa, ni hatua ninayojivunia – Salma Hemed 

Miongoni mwa malengo 17 endelevu ya umoja wa Mataifa ni lengo namba tano la usawa wa kijinsia linalolenga kuwainua na kuwasaidia wanawake na wasichana. Pwani mwa Kenya Salma Hemed ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa shirika la Haki Africa, amejitwika jukumu la kuhakikisha kuwa wanawake wanapata haki hasa zile zinazohusu urithi na uteuzi wa nyadhifa tofauti serikalini na pia  kwa vijana ambao mara nyingi hujipata katika mgogoro na serikali. Katika mazungumzo haya na mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi, Salma Hemed anaanza kwa kueleza alivyoingia katika harakati hizo.

Sauti
3'36"
Dr.Sixbert Mwanga

Wanahabari wafundwa uandishi wa malengo endelevu

Wanahabari wa kada mbalimbali nchini Tanzania, wamepatiwa mafunzo juu ya malengo namba 6, 7 na 13 ya maendeleo endelevu, kupitia shirika la Climate Network Tanzania, CAN lenye ufadhili wa mashirika ya umoja wa mataifa ikiwemo lile la mpango wa maendeleo, UNDP, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi nchini Tanzania. Anold Kayanda amefuatilia mafunzo hayo na  kuandaa makala hii ambapo , Sixbert Mwanga mkurugenzi wa shirika hilo, anaanza kwa kuzungumzia msaada wa umoja wa mataifa katika kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu-SGDs.

 

Sauti
3'40"