Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/UN0118457/

Mimba za utotoni sio kupenda kwetu – Wasichana Morogoro

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto – UNICEF, ndoa za utotoni ni zile zote zinanofungwa kabla ya wanandoa kufikia umri wa miaka 18, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Japokuwa sheria zinapinga ndoa hizi, lakini tabia hii mbaya bado inaendelea ulimwenguni kote. Mbaya zaidi kuwa mara nyingi mimba hizo zinakatisha haki ya elimu kwa watoto hao kwani hushindwa kuendelea na masomo kutokana na sera na sheria za nchi zao. 

Sauti
3'51"
© World Bank/Arne Hoel

Elimu yangu ya Chuo Kikuu nimeihamishia katika ufugaji wa kuku – Veronica Kyalo 

Kama ambavyo lengo namba 8 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, linazungumzia kazi bora na ukuaji wa uchumi, Veronica Kyalo wa nchini Kenya, pamoja na kuwa miaka nane iliyopita tayari alikuwa na elimu ya juu baada ya kupata shahada ya chuo kikuu katika masuala ya uhasibu, hakupata kazi iliyo bora na hivyo hali yake kiuchumi haikuwa nzuri.

Sauti
3'17"
UN Tanzania

Magugu tembo sasa yageuka muarobaini wa mazingira 

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG unataka serikali, kampuni binafsi na asasi zisizo za kiserikali kujitahidi kuhakikisha nishati mbadala na isiyo haribu mazingira inatumika ili kuepusha uchafuzi wa mazingira na ukataji hovyo miti unaochochea kuenea kwa jangwa. Ni kwa kuzingatia hilo nchini Tanzania kampuni ya Mkaa Mweupe ambao ni rafiki kwa mazingira. Je mkaa huo unatengenezwaje?

Sauti
2'49"
UN/ John Kibego

Mlipuko mpya wa COVID-19 watishia ndoto za vijana Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika hivi karibuni ilionya kuwa awamu ya pili ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 barani humo itakuwa shubiri siyo tu kijamii bali kiuchumi. Nchini Uganda hali hiyo sasa ni dhahiri kwa kuwa takwimu za afya nchini humu zinaonesha  ongezeko la mambukizi kutoka watu 200 mwezi Februari mwaka huu hadi wagonjwa zaidi ya 1,000 kwa siku mwezi Mei na kuilazimu serikali kutangaza maagizo mapya ya kuudhibiti.

Sauti
3'54"
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch

Kijana mchoraji anayetekeleza lengo namba 8 la SDGs

Nchini Kenya, kijana Karinge Mbugua, kwa namna moja au nyingine anashiriki kulitekeleza lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalolenga kazi za staha pamoja na ukuaji wa uchumi. Ni kupitia katika kipaji chake cha uchoraji, amewekeza mud ana ujuzi wake katika kazi hiyo ya staha ambayo inamsaidia kukuza uchumi wake. Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amemhoji Karinge na kwanza anaeleza alivyoanza. 

Sauti
3'19"
UN/ John Kibego

Wakimbizi wakaribisha juhudi za UN Women kuwezesha wanawake, Uganda

Nchini Uganda jamii ya wakimbizi katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali wamekaribisha mradi wa kuwawezesha na kushughulikia mizozo katika jamii hiyo unaotekelezwana shirika la National Association oF Professional Environmentalists (NAPE), kwa msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN-Womnen. Mwandishi wetu John Kibego amezungumza na walengwa wa mradi huo wa miaka miwili ambao pia utawanufaisha wenyeji walioko katika makazi ya wakimbizi wa ndani ya Rwamutonga na Kigyayo. Je, wakimbizi wenyewe wanataka ujikite katika masuala gani?

Sauti
3'40"
UN SDGs

Raia wa Uganda wahimiza bunge jipya kuzingatia utekelezaji wa SDGs

Serikali kote dunani zina mchango mkubwa katika utekelezaji wa malenngo ya maendeleo endelevu au SDGs. Nchini Uganda viongozi wa ngazi mbalimbali wa kisiasa wameapishwa  baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amevinjari kusaka yale ambayo raia wa Uganda  wanatarajia wabunge hao kufanya ili malengo ya maendeelo endelevu yafikiwe katika muongo huu wa mwisho kuelekea mwaka 2030. Ungana naye katika makala ifuatayo.

Sauti
3'31"
UN/ Jason Nyakundi

Ndugu watatu wa kiume wajikimu kwa kazi ya ufundi nchini Uganda

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 61 ya watu walioajiriwa duniani, wanapata kipato chao kupitia ajira katika sekta isiyo rasmi. Kwa bara la Afrika, asilimia 85.8 ya ajira zote ni katika sekta hiyo isiyo rasmi ambapo Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya waajiriwa huko ni wanaume.

Sauti
3'55"