Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Najivunia kuwa mfanyakazi wa UNICEF Tanzania kwa karibu miaka 20:Said Mumba

Najivunia kuwa mfanyakazi wa UNICEF Tanzania kwa karibu miaka 20:Said Mumba

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF mwezi huu limetimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake rasmi tarehe 11 Desemba 1946 jijini New York Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. 

Na kwa miaka 75 limekuwa likitoa huduma mbalimbali za kibinadamu na misaada ya maendeleo kwa watoto katika maeneo na nchi 192 na ni moja ya mashirika yanayotambulika na kuthaminiwa kote duniani. 

Miongoni mwa nchi linakohudumu shirika hilo ni Tanzania ambako leo tunakutana na mmoja wa wafanyakazi Said Mohammed Mumba ambaye amekuwa dereva wa UNICEF kwa takriban miaka 20, anatueleza safari yake na jinsi anavyojivunia kuwa miongoni mwa wafanyakazi wa shirika hilo.

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
2'5"
Photo Credit
UNICEF TANZANIA