Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/ John Kibego

"Ningekuwa mbali katika muziki isingekuwa vita" – Mkimbizi nchini Uganda

Katika kuchagiza amani na upendo miongoni mwa wakimbizi, kijana Fideli Karafuru Busimba mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anatumia kipaji chake cha usanii kusambaza ujumbe wa upendo na amani hasa wakati huu wa changamoto zinazotokana na mlipuko wa COVID-19 akiwa ukimbizini nchini Uganda. Kijana huyu ambaye pia ana ujuzi wa uchoraji na useremala, anaomba kupatiwa hifadhi katika nchi ya pili ukimbizini akiamini kuwa itamsaidia kuepuka changamoto za kifedha zinazokwamisha ndoto zake katika maisha.

Sauti
3'42"
UNICEF

Wanafunzi wenye ualbino waona nuru, ni matunda ya azimio la Durban

Tarehe 22 mwezi huu wa Septemba viongozi wa nchi na serikali wanaohudhuria mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa watashiriki mkutano wa ngazi ya juu wakimulika miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio la Durban la kupinga aina zote za ubaguzi ikiwemo rangi na makundi mbalimbali kama vile watu wenye ualbino. Nchini Tanzania hatua zimechukuliwa na sasa kuna mazingira rafiki kwa watu hao kama anavyosimulia Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, nchini humo alipotembelea mkoani Mwanza.

Sauti
4'1"
UN News/ John Kibego

Tafuteni fursa badala ya kuangalia tu madhara ya COVID-19 – Mzee nchini Uganda

Je, wafahamu kwamba kuna fursa kati ya changamoto zilizosababishwa na mlipuko wa covid-19 duniani? Wakati baadhi ya watu wamevunjika moyo baada uchumi kudorora huku wengine wakikabiliwa na changamoto za malazi na upatikanaji wa chakula katika maeneo ya mijini, bado kuna matumaini ya kufanya makubwa zaidi ikiwemo uvumbuzi utakaosaidia hata baada ya corona.

Sauti
3'33"
World Bank/Sue Pleming

Ninaona nilichelewa kutambua umuhimu wa mazingira, sitaki itokee hivyo kwa wengine- Anita Soina

Anita Soina wa nchini Kenya, msichana mwenye umri wa miaka 20 anasema anajiona ni kama alichelewa sana kujiunga katika harakati za kuyatetea mazingira ya ulimwengu. Anita Soina anaona kuna umuhimu mkubwa watoto kufahamu mapema katika umri mdogo kuhusu umuhimu wa mazingira bora ya ulimwengu na namna uharibifu wa mazingira unavyoweza kuhatarisha mstakabali wao. Kutokana na mtazamo huo, sasa Anita Soina yuko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa vijana na hata watoto wamefunzwa umuhimu wa kutunza mazingira.

Sauti
3'34"