Ninarejesha upendo kwa jinsi nilivyosaidiwa nikiwa msichana katika umaskini mkubwa - Dkt Esther Muiu

Ninarejesha upendo kwa jinsi nilivyosaidiwa nikiwa msichana katika umaskini mkubwa - Dkt Esther Muiu

Pakua

Dunia ikiwa katika muongo wa mwisho wa kuelekea katika kilele cha hatua za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, Umoja wa Mataifa umeendelea kutoa wito kwa kila mmoja katika ngazi yoyote kuendelea kufanya juhudi za kuyatimiza malengo hayo 17 ifikapo mwaka 2030.

Nchini Kenya, mwalimu mstaafu mwenye umri wa miaka 76 hivi sasa, Dkt Esther Muiu, tangu mwaka 1999 alipostaafu kazi yake ya ualimu aliyoifanya kwa miaka 40, aliamua kushiriki katika kuyafikia malengo mbalimbali ya maendeleo endelevu kupitia angalau malengo mawili la 4 na la 5 yaani Elimu Bora na Usawa wa Kijinsia. Mwalimu huyo alianzisha shule ya kuwasaidia wasichana kutoka katika familia zisizojiweza kiuchumi ili waweze kupata elimu ya upili au sekondari, kazi ambayo anaendelea nayo hadi hivi leo.

Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amezungumza naye.  
 

Audio Credit
Jason Nyakundi
Sauti
4'3"
Photo Credit
UNEP/Cyril Villemain