UNDP na TAHA nchini Tanzania wajenga vituo vitano vya kuhifadhi na kufungasha mazao
Umoja wa Mataifa unapigia chepuo mifumo sahihi ya chakula inayolenga kuongeza mnyororo wa thamani kuanzia shambani hadi kwa mlaji. Hatua hii siyo tu inasaidia kutokomeza njaa bali pia inaongeza kipato kwa mkulima na ustawi kwa mlaji kwa kuwa zao ambalo linapatikana eneo moja la dunia linaweza kusafirishwa katika ubora wake na kufikia eneo lingine la dunia katika ubora huo huo.