Matunda ni lishe muhimu katika mlo wa kila siku
Emmanuel Mwanjisi ni Afisa lishe kutoka hospitali ya Consolatha, Ikonda, katika wilaya ya Makete, nyada za juu kusini mwa Tanzania, akieleza faida za ulaji wa mbogamboga na matunda katika mwili wa binadamu ameeleza kuwa wataalamu wa lishe wanapohamasisha ulaji wa matunda hawamaanishi kuwa ni lazima mlaji ale kiasi kikubwa cha matunda hayo bali kiasi chochote hata kipande kidogo lakini mara kwa mara, kinasaidia kuleta faida mwilini.