Hii leo katika Habari za UN mwenyeji wako akiwa Assumpta Massoi tunamulika ugonjwa wa kisukari barani Afrika, jawabu la nishati salama Malawi, vijana na wito wao huko Sharm el- sHeikh kwenye COP27 na ujumbe wa Balozi mwema wa IFAD Sabrina Dhowre Elba.
1. Wakati dunia ikiadhimisha hii leo siku ya kisukari duniani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti tishio lake, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO.