Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 NOVEMBA 2022

09 NOVEMBA 2022

Pakua

Karibu katika jarida la Habari za UN hii leo ambalo kwa kiasi kikubwa linamulika harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na wakati huo huo hatua za kuchukua wakati huu ambapo mabadiliko ya tabianchi yanaathiri jamii mbalimbali duniani.

  1. Takriban nusu ya vijana barani Afrika wamesema wanafikiria upya suala la kupata watoto ama la, kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa mujibu wa ripoti mpya ya matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF bakwa kuwahoji watu 243,512 duniani kote.
  2. Miradi mbalimbali ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira inasaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama. Nchini Haiti Shirika la Benki ya plastiki linaendesha mradi wa kukusanya plastiki ikiwa ni moja ya njia za kuboresha afya ya na pia ni chanzo cha mapato kwa wakusanyaji taka. 
  3. Makala: Leo tunakwenda nchini Zambia ambako kijana mmoja amegeuza taka za mabaki ya shaba kuwa mtaji wa nishati salama kwa jamii yake isiyo na kipato!
  4. Mashinani: Tunabisha hodi Sharm el-Sheikh nchini Misri kunakofanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi na nakuunganisha na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM António Vitorino akiwapa ujumbe maalum washiriki wa mkutano huo 
Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
13'13"