Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 NOVEMBA 2022

15 NOVEMBA 2022

Pakua

Leo katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa tunakuletea Habari kwa Ufupi zikimulika idadi ya watu kufikia bilioni 8, Mada kwa Kina tunakupeleka Peru kumulika wanawake wa jamii ya asili na upandaji miti, na Mashinani tunamulika polisi wa Umoja wa Mataifa na ulinzi wa amani.

1. Habari Kwa Ufupi:

Idadi ya watu duniani leo  15 Novemba 2022 inatarajiwa kufiukia watu bilioni 8, ikiashiria hatua kubwa zilizopigwa katika masuala ya afya ambazo zimesaidia kupunguza hatari ya vifo na kuongeza umri wa kuishi limesema shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani na masuala ya afya ya uzazi UNFPA

Leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO limezindua muongozo mpya wa kuboresha uhai na matokeo ya kiafya ya Watoto wanaozaliwa njiti kabla ya wiki 37 au wenye uzito wa chini ya kilo mbili na nusu wakati wa kuzaliwa. 

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya ufuatiliaji wa masuala ya haki za binadamu  nchini Ukraine Matilda Bogner amesema katika miezi michache iliyopita wamewahoji wafungwa w vita 159 wakiwemo wanaume 139 na wanawake 20 ambao wanashikiliwa na serikali ya shirikilo la Urusi na 175 wote wanaume wanaoshikiliwa na Ukraine. 

2. Mada kwa kina: tunafunga safari hadi Peru huko Amerika ya Kusini kwa wanawake wa jamii ya asili waliochukua hatua kulinda misitu kwenye eneo lao.

3. Mashinani: Tutamsikia Mkuu wa Operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoj awa Mataifa Mataifa Jean-Pierre Lacroix akieleza kuwa changamoto mpya na za kipekee zinahitaji polisi wa Umoja huo wajipange upya ili waweze kukabiliana nazo.

Mwenyeji wako leo ni Assumpta Massoi, karibu!

 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'12"